Skip to content

Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?

2019-03-22

Author: By Nsajigwa I.Mwasokwa (Nsajigwa Nsa’sam) with Lucas A. Isakwisa

Numbering: Issue 1.B, Idea: African Freethinking

Place of Publication: Langley, British Columbia, Canada

Title: African Freethinker

Web Domain: http://www.in-sightjournal.com

Individual Publication Date: March 22, 2019

Issue Publication Date: TBD

Name of Publisher: In-Sight Publishing

Frequency: Three Times Per Year

Words: 7,696

ISSN 2369-6885

UTANGULIZI

Karibuni tena Wandugu. Sisi ni Jamaa Watafiti wa Jichojipya-Think Anew, Taasisi iliyosajiriwa rasmi yenye malengo ya Kielimu ya kueneza elimu ya falsafa kwa ujumla, kuondoa hofu ya kufikiri na kuchochea FikraHuru kwenye jamii kwa lengo la kuwa na mabadiliko chanya ya enzi za Mwangaza (enlightenment) katika jamii, kwa kutumia njia ya urasini – mantiki na ushaidi (rationalistic, logic, empirically-based secular values)…

Kazi yetu ya kujitolea tunayoifanya;- Kuwatambua, Kuwaibua na Kuwaunganisha Watanzania ambao ni Wanafikra huru – freethinkers…hawa ni wale wasio-ogopa kujiuliza maswali mwanzo mwisho, wanaofikiri nje ya box la mazoea ya utamaduni mila na desturi zake, ikiwa ni pamoja na utamaduni wa dini. Kwa kimombo hawa ni Freethinkers, Rationalists, Sceptics, Secular Humanists, Agnostics and Atheists, wanaoishi kwa “Maadili bila dini”. Jichojipya ndio tuliofanya mahojiano ya kifalsafa na Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru wakati wa uhai wake (tafuta kwa google makala hii – Mahojiano yaliyogeuka kuwa majadiliano na Kingunge Ngombale Mwiru Mkongwe Mwanafikrahuru wa Tanzania) na alitueleza kuwa yeye alikuwa ni Mwanafikra huru (independent thinker and a freethinker) ikiwa ni kinyume na watu walivyomkisia. Ilikuwa siku ya nadra mahojiano yale, na inakuwa nadra tena ambapo tumepata wasaa mwingine kufanya mahojiano na Mtanzania mwingine kwa jina, Profesa Alex L Mwakikoti, ambaye anayaishi maisha yake kama ya falsafa ya Kingunge Ngombale Mwiru, yakiwa ni sawa pia na yule Profesa na Mwandishi maarufu wa vitabu, Okot p’Bitek, aliyeandika kitabu cha “Song of Lawino and Okol”, pia utafiiti wake katika kitabu “African religions in western scholarship” na pia “Towards Africa’s cultural revolution”. Okot p’Bitek kutoka kanda yetu ya Africa Mashariki (alikuwa Mganda) alifunguka waziwazi kuwa yeye ni Mwanafikra huru aliyeishi bila dini…vile vile Profesa na mwandishi wa vitabu wa Nigeria Afrika magharibi Wole Soyinka, mshindi wa kwanza toka Afrika kwa tuzo ya Nobeli (1986) kwa upande wa uandishi/lugha, aliyeandika kitabu “The Trial of brother Jero” na vinginevyo.

Jee inawezekana kuishi kwa Maadili bila dini..? Tusome mahojiano haya kujua hilo,

Mwalimu Prof Alex Mwakikoti, sisi ni Jichojipya-Think Anew, tuna furaha sana kuwa na wewe, karibu sana…

                                                              MASWALI NA MAJIBU

An Interview to a Tanzanian Emeritus Professor Alex L. Mwakikoti on Living Without a Religion and More Scott Douglas Jacobsen In-Sight Publishing

Wana fikrahuru wa Jichojipya Tanzania, Nsajigwa Mwasokwa (kushoto) na Prof Alex Mwakikoti (kulia).

1) ( a) Mwalimu Profesa, wewe ni MwanafikraHuru (an independent thinker and a Freethinker), kwani ni nini, yamaanisha nini kuwa hivyo..?
(b) Ilikuwaje mpaka ukafikia hatua hiyo ya kuwa MwanafikraHuru? ni nini kinachosababisha mtu kama wewe kuwa MwanafikraHuru? Ulikuwa hivyo katika umri gani? Tunaomba tujue maisha yako kwa upande huo Mwalimu.

Profesa A Mwakikoti:  Asante sana kunikaribisha.  Ninachoweza kusema ni kuwa, MwanafikraHuru ni yule ambaye hawi na uegemezi, hakwazwi katika kufikiri kuhusu suala lolote; akitumia njia ya urasini – mantiki (Rationalism). Ni tabia ya toka utoto ya kujiuliza maswali kwa udadisi wa kutaka kujua tu. Bahati mbaya sana tabia hiyo ya utotoni, taratibu inafutika jinsi wengi wetu tunavyokua wakubwa kwa kuwa, njia zetu za kufikiri (mental capacity) zinakuwa zimejengeka kutokana na tamaduni na desturi za jamii zetu ambazo tunajikuta tumekulia.  MwanafikraHuru kwa uelewa wangu, ni yule mtu ambaye, baada ya kujengwa na malezi ya jinsi ya kufikiri juu ya  tamaduni na desturi ya makuzi ya mahali alipokulia, anarudia tabia ya udadisi ya utotoni na kujiuliza maswali, lakini sasa akiwa na uhuru wa kuuliza juu ya chochote hata yale ambayo jamii imefundisha kuwa ni “hatari” kujiuliza (yasiulizwe). Na kwa kuwa sasa yeye ni mtu mzima, hakuna tena mipaka ya kumzuia asiulize na kutafuta majibu kwa maswali hayo (yasiyoulizika) katika jamii. Hakuna tena cha kumzuia kujiuliza. Kwa dunia ya leo, MwanfikraHuru kama huyu anatambulika kuwa Atheist, Agnostic (asiye na dini, asiye na Mungu) au Humanist M-binadamu nk.

Safari yangu mpaka kuja kuwa MwanafikraHuru ilikuwa ni hatua (process). Haikuwa kitu kilichotokea sehemu moja au mara moja ghafla. Ebu niwaelezeni kidogo maisha yangu kwa ufupi.  Mimi nilizaliwa na Muinjilisti / mhubiri mahili wa kanisa la Kilutheri, Yehoswa Mwakikoti – ndiye aliyekuwa baba yangu.  Alikuwa ni mtu aliyejitolea sana kueneza injili eneo kubwa kule Udzungwa mkoani Iringa, Tanzania.  Nikiwa nakua, nilifuata hatua za baba yangu kwa mambo mengi kama alivyoyafanya yeye. Wapo waliotabiri kuwa nitajakuwa Mhubiri kama baba yangu. Nilibatizwa nikiwa mdogo, na baada ya kupata kipaimara (hatua ya kuwa mkristo kamili) nikiwa na umri wa miaka 13 nilianza kujiuliza maswali kuhusu baadhi ya hadithi za kwenye biblia.  Nilizifurahia hadithi hizo, lakini pia niliona zingine zilikuwa ni za matisho sana, na kwa kweli zikaishia kunifanya niwe muoga – mwenye hofu ya adhabu za Mungu kwa wale ambao hawamtii. Nilipomaliza shule ya msingi, nilihisi kanisa la Kilutheri halikufundisha biblia kiusahihi, hivyo mwaka 1967 niliamua kuliacha kanisa hilo lakini sikujua niende kanisa gani. Baada ya kujisomea mwenyewe biblia, niliamua, badala ya kupumzika siku ya Jumapili, nipumzike siku ya Jumamosi ikiwa ndiyo siku ya sabato, kama vile biblia inavyofundisha.  Baadae nilikuja kutambua kuwa kumbe kuna watu wanaitwa Wasabato (Seventh-day Adventists) ambao walikuwa wanafuata mafundisho hayo ya kupumzika Jumamosi. Baadae nilijiunga na kanisa hilo. Nilipomaliza elimu yangu ya sekondari, Mmissionari mmoja toka Marekani aliniuliza kama ningekuwa tayari kujitolea kuanzisha na kueneza kanisa la Wasabato huko Mufindi, Iringa, na kuniahidi angenitafutia/angenipeleka chuoni baada ya hapo.  Nilikubali hilo na kweli Mmissionari naye alitimiza ahadi yake. Nilikwenda kusoma mafunzo ya cheti cha Diploma miaka miwili huko Uganda, nikarudi Tanzania na kufanya kazi kama Pastor huko Lindi and Temeke, Dar es Salaam.  Baada ya hapo nilikwenda kumaliza degree ya kwanza katika somo la Thiolojia katika chuo cha Newbold College Uingereza. Sikutaka kuachia masomo yangu kwa shahada ya kwanza, niliamua sasa kutafuta njia yeyote kujisomesha mwenyewe kwa masomo ya juu.  Ilikuwa nilipokuwa nasoma degree ya pili (Masters) ya somo la Thiolojia ndipo tena hulka ya udadisi ikaibuka tena na kwa nguvu mpya, na nikawa na maswali mengi juu ya biblia na wahusika wake.  Kama nilivyokwisha sema, siwezi nikaisema siku moja hasa ya kubadilika kwangu na kuwa MwanafikraHuru, ila ninachoweza kusema ni kuwa baada ya kumaliza shahada ya juu – PhD kwenye somo la Sociology – ustawi wa jamii, maswali zaidi yakazidi kuibuka, hasa pale nilipojifunza kuwa kumbe ni jamii yenyewe ndiyo inayounda dini, na sio dini inayounda jamii. Hatimaye mwaka 2007, niliachana na dini zote, nikajiita Humanist, M-binadamu.  Waweza kusema nilikuwa MwanafikraHuru na M-binadamu (Humanist) nilipokuwa katika kilele cha kazi yangu profesheni kama Mwalimu, Profesa wa somo la ustawi wa jamii (sociology) na mawasiliano (communication).

Jichojipya – Think Anew: Ahaa, Mwl Profesa, umekumbusha kabisa mahojiano yetu na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (Tafuta kwenye google“Mahojiano yaliyogeuka majadiliano na  Kingunge Ngombale Mwiru Mkongwe Mwana fikra huru wa Tanzania ”). Naye alisema safari yake kama vile yako wewe, kwamba alikuwa anajiuliza maswali juu ya imani yake tokea anakua ngazi zote shuleni, na ni pale aliposoma vitabu vya falsafa, cha Thomas Paine na hasa kile cha Ludwig Feuerbach (tafsiri yake kwa kiingereza “The “Essence of  Christianity”) ndipo alipong’amua alaa, hivi kumbe siyo kuwa Mungu kamu-umba binadamu kwa mfano wake ila ni kuwa binadamu ndiye kamu-unda Mungu kwa fikra zake mwenyewe…kwamba kumbe ni jamii ndiyo inayounda Miungu yake…kuanzia pale naye akawa MwanafikraHuru..!

2) Mwl Profesa, nini uzoefu wako wa kuwa MwanafikraHuru? Utakuwa umeishi maisha ya upweke sana sivyo..?  una akili sawasawa..?

Prof A Mwakikoti:  Mimi kama MwanafikraHuru (independent thinker and a freethinker), niliona / nilijihisi jinsi nilivyokuwa mpweke.  Marafiki zangu wengi walikuwa ni watu walio kwenye dini, wengine waliozama ndani ya dini sana, wakiwemo wana familia yangu, hasa mke wangu. Nakumbuka sana maongezi ya uzuni kati yetu, nilipoamua kuwa MwanafikraHuru wa wazi hadharani- public, bila kificho (an open freethinker).  Biblia yafundisha kuwa watu wenye imani tofauti wasioane, tutaishije maisha yetu baada ya ukweli huu kuwa mmoja wetu sasa haamini tena mambo ya dini – ni MwanafikraHuru?  Tulifikia muafaka ya kuwa, kila mmoja wetu ataenda njia ya imani yake lakini tutabaki kwenye ndoa yetu. Hii ina changamoto yake.  Kwa sasa sijioni mpweke kuwa MwanafikraHuru.  Kutokana na tekinolojia ya mawasiliano ya sasa, Intaneti inaleta taarifa mbalimbali na links – makutano kwenye mtandao kwa makundi ya aina mbalimbali. Ilikuwa ni kwa njia hiyo ya mtandao nilipokuja kujua kuwepo makundi mengine ya WanafikraHuru – Freethinkers – Atheists -Humanists. Nilifurahi sana nilipokutana kwenye mtandao na Nsajigwa Nsa’Sam Mwasokwa, na kuelewa kuwa, kumbe yawezekana kuanzisha rasmi taasisi ya WanafikraHuru – freethinkers Tanzania, ambayo ninajivunia kuwa mmojawapo katika kuwezesha kuwepo kwake rasmi toka hatua za mwanzo.  Kwa sasa “sipo tena peke yangu”,  Na kiakili, kimawazo na kihisia, na uhusiano wangu na WanafikraHuru wengine wenzangu ni nzuri kuliko nilivyoanza safari yangu. Nipo vizuri.

Jichojipya-Think Anew: Profesa, Ni Nsajigwa huyu huyu au kuna mwingine..?
Prof A Mwakikoti…Ni huyu huyu Nsajigwa wetu…yeye kwa kweli ndiye Pioneer kwa wakati wa kizazi chake na cha chini ya hapo, ukienda kwenye mtandao kutafuta habari za FikraHuru Tanzania, Nsajigwa Nsa’Sam Mwasokwa atakuwa ndio wa kwanza kutokea…WanafikraHuru Tanzania tunajivunia Nsajigwa mmoja wetu.

ALL PICHA FROM TABLET KUBWA 1077

Waasisi wa Taasisi ya Wanafikrahuru Tanzania, Jichojipya, Profesa Alex Mwakikoti (kushoto) Nsajigwa Nsa’sam Mwasokwa (katikati) na Wakili Isakwisa A Lucas (kulia).

3) Jee wasomi wenzio (Academicians) walikuchukuliaje (kisomi, kijamii, kidini) kwa wewe sasa kuwa MwanaFikraHuru? Hakukuwa na unyanyapaa kwa aina yoyote..?
Na umesema umeshiriki uanzilishi wa Jichojipya -Think Anew, tueleze ulikuwaje Mwanajichojipya  – Think Anew, na uzoefu wako ndani ya Jichojipya ni upi? Unaonaje kazi ya Jichojipya mpaka sasa, na matarajio yake baadae..?

Profesa A Mwakikoti:  Kwanza nilikuja kujua kuwa kumbe katika chuo – University of Texas kilichopo Arlington, ambapo nilifundisha kabla, kulikuwa na tawi la Wanafikrahuru – Atheists; laiti ningelijua wakati nipo pale, ningekuwa nimekwisha jiunga nao kuwa mwanachama mara moja.  Waalimu wasomi ngazi ya juu Marekani (Academicians), wanamkubali mtu bila kujali dini au kutokuwa na dini.  Ni muendelezo wa katiba ya nchi ya Marekani kwamba, shirika lolote pamoja na vyuo, haviwezi kubagua mtu yeyote kwa sababu ya imani yake au kutokuwa na imani yoyote ya dini. Lakini ni kweli pia kuwa unaweza kujihisi kutengwa kunapokuwa na matukio/sherehe za kidini, ila sasa pia vyuo vikuu vingi vinatofautisha matukio hayo ya kidini nje ya utendaji wa kila siku wa vyuo, kama vile ambavyo kuna kutofautisha mambo ya kanisa (dini) na yale ya dola/serikali. Ingawa pia nilipofundisha chuo kilicho chini ya taasisi ya kidini – a religious affiliated institution (Wiley College), kulikuwa na hali ya mvuto kumfanya mtu yeyote pale awe mmoja wao, achanganyike katika desturi hiyo (ingawa pia hawakumlazimisha/hawakumshurutisha mtu) kwani wangekwenda kinyume na serikali.  Ninakumbuka tukio ambapo Chaplain wa chuo aliniomba nishiriki mada na zungumzo kwenye assembly ya chuo.  Nilipomueleza mimi sifungamani na dini yoyoye, aliniomba niseme tu kitu chochote, sababu alisema, “wanafunzi wengi wa faculties – vitengo mbalimbali hapa chuoni wanakuheshimu sana”. Niliamua kukubali ombi lake, na kwa uzoefu wangu wa elimu yangu ya Thiolojia nikazungumzia somo toka kwenye biblia, “ukweli utakuweka huru.” Alifurahi kuona nimeleta mtazamo ambao wengi kwenye dini hawafikirii sana juu yake, akili ya utoto ya kujiuliza maswali kuufikia ukweli.  Ukiwa kwenye Taasisi yenye muegemeo wa kidini, MwanafikraHuru unatafuta njia kwa fursa inapopatikana kama ile, kuelezea tunautafutaje na kuufikiaje ukweli.  Nakumbuka baada ya maongezi yale, wanafunzi wawili walinijia na kuniambia nao pia ni wasioamini dini (freethinkers nonbelievers) na walishangaa sana kujua mimi ni mmoja kama wao!

Na pia kama nilivyokwisha sema, ilikuwa wakati najiuliza na kutafuta kwenye mtandao kama kuna Wanafikrahuru – freethinkers wowote Tanzania ndipo nikakutana na jina Nsajigwa Nsa’Sam Mwasokwa. Baada ya mawasiliano ya muda mfupi, niliamua nitamtafuta tukutane ana kwa ana nitakapokwenda Tanzania . . . mengineyo ni historia.  Unaweza fikiria, nilivyokuwa “motomoto” nikitaka tuwe na Taasisi itakayokwenda “mwendokasi”, lakini uhalisia haukuwa hivyo.  Uzoefu wangu kama MwanafikraHuru ndani ya Jichojipya – Think Anew ni kuwa, imekuwa kitu kizuri sana.  Hakika, hamna Taasisi isiyo na changamoto zake; lakini kuwepo kwa changamoto ndio kunawafanya watu wafikiri.  Nikipima shughuli ambazo Taasisi Jichojipya imefanya mpaka sasa, naona ni hatua kubwa, lakini zaidi pia, ninaangalia mbele nikiamini kwa pamoja nini zaidi tunaweza tukafanikisha kama Taasisi. Unaona, mimi kama M-binadamu (Humanist) naona kwamba, kama Taasisi, tunaweza kuleta kile kinachokosekana sasa ktk jamii yetu.  FikraHuru…Elimu, Elimu – Vitendo inayowapa uwezo watu hasa vijana, waweze kuwa wazalishaji kwenye jamii yetu —hasa wawe wajasiliamali katika nyanja mbalimbali.  Ndiyo maana nadhani wakati tunaanza na hatua ndogo ndogo, matarajio na maono lazima yawe kufanya makubwa bila mpaka.  Ninafikra kuwa tunaweza kuunda jamii ambazo zinajitegemea, kuanzia Taasisi yetu wenyewe (Jichojipya) inayoweza kuzalisha mali na kusaidia jamii kwa wahitaji kwa njia tofauti mbalimbali, kama vile elimu, afya, kipato na mengineyo.  Hivyo ni lazima, ni budi kwetu kupanga ramani ya wapi tunataka kwenda na kufika katika miaka mitano, kumi, ishirini na hamsini kuanzia sasa.

4) (a) Mwl Profesa, Wewe ni MTanzania msomi uliyebobea wa elimu jamii – sociology…jee uliwahi kukutana na pengine kujadiliana na Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere? (b)Vipi kuhusu hili ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliposema (katika mojawapo ya hotuba zake) kwamba ikitokea tutamchagua Mtanzania asiye na dini – ambaye si muumini wa ukristo au uislamu kuwa Rais wa Nchi, tutatafuta utaratibu mwingine wa kumuapisha, bila ya biblia au Koran…jee unasemaje kwa hili la Mwalimu..?

Profesa A Mwakikoti:  Kwa bahati mbaya sikuwahi kukutana na Mwalimu J. K. Nyerere ana kwa ana, ila nimesoma maandishi yake na kusikiliza hotuba zake.  Muda wote nashangazwa kwa kweli kwani yeye alikuwa mjumuishi – inclusive bila ubaguzi, kwenye fikrahuru na maono yake kwa nchi ya Tanzania na kwa Watanzania.  Kwa mfano wake wa kauli hiyo ya kuangalia mbele, kwamba ije siku ambayo kumchagua mwongozi wa nchi ambaye hata kuwa na dini.  Hii inaonyesha jinsi alivyokuwa na upeo mkubwa wa kuona mbele kwa uwezekano huo wa wapi Tanzania itaweza kujikuta imefika siku moja, mbeleni. Kwa kauli hiyo yaonyesha wazi alivyo Kiongozi mwenye maono na busara.

Jichojipya – Think Anew: Ila lakini pamoja na wewe kuto-kukutana naye ana kwa ana, jee unadhani mafundisho/falsafa yake imekushawishi – influence wewe kwa namna yoyote ile..?

Profesa A Mwakikoti…Ndiyo…hasa mawazo yake kuhusu Elimu ambayo ni kama yale ya Paulo Freire wa Amerika ya Kusini – kwenye kitabu Pedagogy of the oppressed. Elimu isiwe nadharia tu, bali iende na vitendo, isiwe “elimu kwa minajiri ya elimu tu”.

(c) Profesa,  Kwingine wapi, ikiwa nje ya hivyo vitabu (vya dini), mtu ambaye ni MwanafikraHuru asiye muumini wa hivyo, atapata maadili..?

Profesa A Mwakikoti:  Nikiwa ni mmoja wapo niliyekuwa ndani sana kwenye dini, naweza kusema kwa ushuhuda kuwa, hivyo vitabu vinavyoitwa vya dini, mfano biblia, havina ulazima wa maadili ambayo mtu atayategemea kumuongoza.  Hivi unaelezaje kwa mfano, maadili ya kulazimisha mtu akuabudu na asipofanya hivyo unamuadhibu?  Vipi unawezaje kulazimisha upendo kwa mtu? Jee hayo ni maadili..?  Ni vipi unamuadhibu au kumuua mtu ambaye hajafanya kosa lolote, ila kwa niaba ya mwingine aliyefanya kosa..?  Achilia mbali hadithi za mauaji mengi kama yalivyo kwenye vitabu hivyo “vitakatifu”, yaliyohalalishwa (ruksiwa) na mungu..? – Hayo kweli ni maadili..?  au la vinginevyo, hivi tunapo-maanisha “maadili” tunazungumzia nini hasa? Kutokana na uzoefu wangu, ninaweza kuwa shuhuda kwamba, ni baada ya kuachana na dini ndipo nilipoona inawezekana na ni asilia kabisa kuwa na maadili bila dini – ‘good’ without a god.  Kufanya mema kwa uhuru bila tazamio la zawadi au woga wa adhabu. Upendo wa kweli unapatikana pale ambapo unafanyika kwa uhuru bila masharti.

(d) Ingawa Watanzania kama Waafrika wengi wapo kwenye dini sana “notoriously religious”, (kwa maneno ya  Profesa John Mbiti) lakini Tanzania ni nchi isiyo na dini (yaani ni “secular state”) kwa katiba yake na pengine kwa uenendaji (practice) wa katiba hiyo. Wewe kama MwanafikraHuru, una maoni – uchambuzi gani kuhusu hili…ni kwa kiasi gani ni kweli kikatiba na kivitendo?
Jee hudhani kwa namna moja au nyingine, kuna mgongano ambapo wakati mwingine dini inajipenyeza kwenye mambo ya dola/serikali Tanzania?

Profesa A Mwakikoti:  Ingawa nadhani Profesa John Mbiti ali rahisisha – simplify sana uhalisia wa Waaafrika kwa kufikiri kwamba kwa kuwa Waafrika walikuwa na imani za kiasili – faith traditions, basi walikuwa wenye imani sana ‘notoriously religious’.  Anaweza kuwa sawa kwa maana ya kuwa, Kanuni fulani (principles) zinarithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine –  iwe ni desturi za kidini au zinginevyo. Hiyo ni asili tu kwenye jamii (natural societal dynamics).  Lakini pia huwezi kuyaweka yote hayo kwenye kapu moja na kusema ni dini. Jamii yenyewe kwa makusudi / kusudio – consciously ndiyo inatengeneza  dini kupitia kwa kiongozi mwenye mvuto – notorious charismatic leader kueneza na kuendeleza ujumbe (kama wao binafsi, au la wakisema/wakifikiriwa / ikiaminishwa kuwa wametumwa na Mungu.  Lakini pia Mbiti kwa kauli yake hiyo (kuwa Waafrika ni “notoriously religious”) yaweza kuwa ilikuwa ni njia yake ya ku challenge – kukinza dhumuni la watu toka magharibi wakija Afrika na picha ya “kuleta dini kwa wasio na dini – wapagani”.  Pale desturi au dini inapotengenezwa na jamii, inarithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, na ni wazi inaweza kuathiri Taasisi zingine katika jamii ikiwemo dola na serikali yake. Kumbuka kuwa serikali zote zinatokana na (ni matokeo ya / zinatengenezwa na) jamii.

(e) Mawazo yako Profesa kwa  “Dua la kuliombea Bunge”, na pia wimbo wa Taifa ambapo kwa yote hayo Mungu anatajwa wakati Taifa/dola ni secular – halina dini, siyo theocracy…vipi hii Profesa, siyo utata, kujichanganya..?)

Profesa A Mwakikoti: Jamii nyingi, ikiwemo ile inayosemekana ni huru sana (Nchi ya Marekani) bado zina struggle – hangaika inapokuja hilo la desturi ya dua, au kuwepo neno Mungu kwenye nyimbo zao za Taifa na kwenye kula kiapo cha ofisi.  Binafsi nina amini ni kutokana na nguvu (dynamics) za jamii. Watu wengi katika jamii si Wakushuku, Wadadisi (not critical thinkers)—Yahitaji nguvu ya ziada kuwa MwanafikraHuru.  Kwa wengi, tunachukulia vitu kama vilivyo bila kujiuliza maswali juu ya huo utamaduni mila na desturi tunazofuata, kwa kurithishwa.  Hapo ndipo penye utata —sisi kweli ni secular? – bila dini au ni theocracy – ndani ya dini?  Ikiwa ni Tanzania au Marekani, kwangu mimi huu ni utata.

Jichojipya – Think Anew: Kwa hili hata Mwalimu Nyerere aliwahi kulizungumzia kwenye moja ya hotuba zake. Naye aliona ni “utata” tunaposema nchi haina dini wakati huohuo wimbo tunasema “Mungu ibariki”..!

5) Profesa, Wewe kama MwanafikraHuru (a freethinker) wa muda mrefu, tunaomba utueleze uzoefu wako;- nini uzuri wa kuwa MwanafikraHuru? Na pia nini changamoto zake..?

Profesa A Mwakikoti:  Mimi kama MwanafikraHuru, ninapenda kuangalia vitu kwa hulka ya usawa / hakisawa na uhuru (fairness and freedom).  Pamoja ya kuwa si muda mrefu sana, nimependa ile hali ya kuwa Mhusika – responsible wa maamuzi yangu ninayoyachukua, bila ya kumuogopa kiumbe aliye mahali (sijui wapi) ambaye atanipa zawadi au adhabu kwa fikra na matendo yangu. Ninajitegemea!  Hali hii ya fikra imeniweka huru kweli.  Huu ndio uzuri wa kuwa MwanafikraHuru. Siogopi vitisho vya moto wa milele huko kuzimu.  Changamoto kwangu ni kuwa mwenzangu mke wangu ambaye yeye ni muumini wa dini.  Inanibidi nifikirie sana kabla ya kufanya vitu fulani ili nisim-kere. Lakini sasa pia, mimi kama MwanafikraHuru ambaye ninaishi kwa Ubinadamu – natanguliza Ubinadamu kwanza. Ninafikiria na wengine pia kwa athari za maamuzi yangu ninayoyafanya. Wakati mwingine hii inapelekea nikubali kufanya muafaka.  Mfano  tunapokuwa na wageni na mke wangu anatutaka tusimame, tufumbe macho na tukiombee chakula; hata kama sifumbi macho, lakini kwa Heshima nitasimama.  Na huo ndio umekuwa utaratibu wangu kwa Taasisi ambazo zinaanza kikao kwa sala.

6) Profesa, Kwa mtazano wako wa  FikraHuru, miaka 50 na ushee ya Uhuru sasa, unaionaje baadae (picha yake) ya Tanzania na Afrika katika suala la Uhuru wa mtu (binafsi) – Liberty na suala la maisha bora?

Profesa A Mwakikoti:  Uhuru na maisha bora ni watu wanaotengeneza hali hiyo.  Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na nchi zinginezo za KiAfrika iwe ni mwanzo wa tafakari na mipango kwa miaka mingine 50 ijayo..ni vipi Afrika na Tanzania ya kesho ije kuwa.  Mwalimu J K Nyerere alifungua njia kwa namna mbalimbali, Wakuu wengine baada yake wamefanya yaliyowezekana kwa wakati wao.
Ni muda muafaka sasa kwa Tanzania na nchi nyinginezo za Kiafrika, kufikiri zaidi nini nchi zao zataka viongozi wake wafikiri ziwe miaka 50 ijayo, na si tu kila mmoja kwa wakati wa kipindi cha miaka yake ya uongozi. Fikra hizo lazima ziangalie uchumi, elimu, kupunguza umasikini, ustawi wa jamii na mengineyo.  Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni tajiri sana kwa rasilimali, ujuzi na nguvukazi za kutosha kutengeneza vitu vyetu wenyewe kwa hitaji lolote na hata kuuza nje vingine vingi. Hakuna sababu kwa kweli kwa nchi zetu kuendelea kutafuta / kuomba misaada kutoka nchi nyingine—ilitakiwa nchi zetu ndiyo zingekuwa zinatoa misaada kwingineko.  Na kukiwa na utoshelevu kwenye uchumi na kwingineko, uhuru na maisha bora vitafikiwa.

An Interview to a Tanzanian Emeritus Professor Alex L. Mwakikoti on Living Without a Religion and More 2 Scott Douglas Jacobsen In-Sight Publishing

7) Profesa, nini maoni yako kama MwanafikraHuru kuhusu (a) kushindwa kwa Tanzania na nchi zingine za Afrika kupata maendeleo ya viwanda, pamoja na juhudi zote za huko nyuma? Na vipi maoni yako juu ya falsafa ya Mwl Nyerere, ya kujitegemea?

Profesa A Mwakikoti: Ninadhani Tanzania na nchi zingine za Afrika zipo kwenye safari ya kujenga uchumi wa viwanda. Ni muhimu hapa kuangalia nyuma na kujifunza kwanini imeshindikana kuwa na viwanda ndani ya miaka 50 ya Uhuru?  Wapo wanaosema ni muda mfupi unapolinganisha, kwa mfano, na Marekani kwa miaka yao zaidi ya 250 ya Uhuru.  Lakini mtu anaweza kujiuliza hili; Ni muda gani ilichukua kwa tekinolojia ya mawasiliano ya simu za mkononi kuenea? Mbona hatukusema tufuate mwendo wa kinyonga (pole pole) kwa hilo, kama ambavyo Marekani ilichukua muda mpaka kuwa na mawasiliano hayo? Mbona kwa hilo tulikwenda mwendo-kasi tukarukia treni mara moja? Nakumbuka nilipokuja Tanzania nikakuta tayari kuna watu hapa walikuwa na simu za mkononi kabla hata ya wengi wetu sisi huko Marekani!). Vitu vinakwenda kasi leo hii, nasi lazima twende (tubadilike) hivyo.  Tuna wajuzi, tuna rasilimali, tuna vifaa vya kuzibadili malighafi kutoka kwenye utajiri wetu asilia, kwanini ichukue miaka mingi mingine?   Mimi nina-amini ni suala la kubadili jinsi tunavyofiikiri, tufikiri upya. Hilo likifanyika, ujenzi wa viwanda na uendelevu wake utakuja kwa haraka zaidi.  Ninaona ya kuwa, msisitizo wa falsafa ya kujitegemea wa JICHO JIPYA kama Taasisi iwe ni kielelezo cha kuchochea kuleta mabadiliko katika jamii yetu ambapo, itaonyesha “forward thinking”  – kuona mbali kwa Mwalimu Nyerere na viongozi wengineo wa serikali kwa sasa.

(b) Kuongezeka kwa  fikra za imani za wakati wa giza – “Dark age attitude” – kuamini katika ushirikina, miujiza, uchawi, msukule, ndondocha, kumchukia bundi, kuwa na “kamati ya ufundi-uganga na ramli” ili kushinda mechi za mpira wa miguu, “ufreemasoni” – kama unavyoelezwa hapa kwetu, mpaka hata mauaji ya watu (hata watoto, na wenye ulemavu wa ngozi) kutokana na imani hizo… Jee, hii ni kiashiria kwamba zile juhudi za Elimu bure ikiwemo ile ya “Ngumbaru” ya watu wazima kupigana dhidi ya “adui ujinga” zilipotea patupu..? Au la, Ni wapi tulikosea?

Profesa A Mwakikoti:  Hizi imani zote za hulka ya “enzi za giza” orotheshwa hapo ninaziona ni kutokana na elimu – ukosekanaji wake.  Kwa Tanzania, nafikiri, vita dhidi ya ujinga haiwezi semwa ilikuwa ni “patupu”, ila tuseme haikuwa yenye uwiano. Swali ni kuwa, elimu izungumzie nini? Elimu ili iweje? elimu ifanye nini? lengo lake liwe nini? Matokeo yake? Kwa kimombo ‘what should education address?’ hili ndio la kuangaliwa sana, kinaga-ubaga, kiutafiti, na Taasisi zote husika (za elimu).
Kwa muda mrefu sana na mpaka hivi karibuni, elimu imefuata utaratibu wa / desturi ya mkondo wa enzi za ukoloni ambao haujatoa masuluhisho ya kutosheleza kwa jamii yetu na wanafunzi wetu.  Mfano, kuna tija gani, faida gani kuwa na vyuo vingi – vya kati na vyuo vikuu Tanzania, vyote vikitoa aina ile ile ya elimu – silabasi ya kikoloni, inayopelekea kuwepo na wanafunzi wengi kuliko, wahitimu wa vitu hivyo hivyo, na hawapati kazi..?  yabidi sasa tufikiri upya – critically rethink mahitaji ya Tanzania ya miaka mitano, kumi na hata ishirini au zaidi toka sasa wakati tuna amua silabasi – curriculum  ya shule zetu.  Vijana wetu wapohitimu shahada zao, wasianze mahangaiko ya kusaka ajira zisizojulikana, za mashaka na hata ambazo ni za uvunjaji wa sheria.  Ni lazima kuweka mazingira ambapo kuna aina nyingi na tofauti za ajira ambazo zimechunguzwa mbeleni (have been carefully forecast) miaka mingi kabla wahitimu hawajamaliza elimu/mafunzo yao.  Hii yahitaji fikra mpya fikra pevu (critical thinking) toka kwa Taasisi zote husika Tanzania, na JICHO JIPYA nayo hakika ni mdau katika hili.  Tukirudi nyuma kidogo, kisomo cha Ngumbaru kilitakiwa, na kinatakiwa kuwa endelevu; si tu kujua kusoma na kuandika, bali na kuambatana na matumizi ya elimu hiyo katika maisha ya kawaida.  Na hili pia linahitaji majibu ya swali la ‘elimu ya ngumbaru kwa lengo gani’.  Tukijua jibu lake, elimu hiyo pia itakuwa ina umuhimu na endelevu.

8) Mwalimu Profesa, Wewe kama MwanafikraHuru, nini ushauri wako kwa  vijana ambao ni WanaFikra Huru Chipukizi? (Wapo hata kama ni wachache, hamna jamii isiyo na watu wanaofikiri nje ya box la mazoea na desturi ya jamii hiyo, hivyo hata hapa Tanzania lazima wapo!) Jee WanaFikra Huru wa Tanzania wanaweza kuwa na mchango chanya wowote katika jamii..? kwa vipi? Jee wanaweza kuwa ni “galimoto” la kuelimisha dhidi ya imani za “enzi za giza” – uchawi, kwa jamii yetu ambayo yaelekea kwa kiasi kikubwa haitumii njia ya fikra ya urasini-mantiki (rationalism)..?

Profesa A Mwakikoti:  Kwa ujumla wake, Vijana ndio waleta mabadiliko katika jamii. Ushauri wangu kwa vijana ambao ni WanafikraHuru ni kuwa, wawe pragmatist – waishi kimatendo kuendana na uhalisia katika maisha yao ya kila siku.  Na wawe mifano kwa wao kuendelea kujifunza wenyewe bila kuchoka kuhusu kila kitu, na kutafuta maelezo na majibu ya urasini mantiki (rationalism) katika hali zote zozote wanazokutana nazo.  Nina imani hii itapelekea galimoto la fikra kuielimisha jamii dhidi ya fikra za imani potofu katika matukio ya kimaisha.  Kwa upande mwingine, tuna bahati Tanzania na nchi nyingine kwingineko kuwa, tayari tuna vijana wenye nguvu na hari, ambao wapo katika nyanja mbalimbali katika jamii, mstari wa mbele wa nyanza hizo.  Tutumie nafasi hii, si kuhubiri ili kubadili watu wafuate njia yako ya kufikiri, la, ila ishi maisha yako, na wengine watataka kujua na kujifunza falsafa gani inaongoza maisha yako na mafaniko yake.

9) Kwa maoni yako Profesa Mwalimu, kama MwanafikraHuru, jee hili la “hulka ya lawama” kwa magharibi,  kwa sasa kete hii bado ina mantiki? – “blame game’ to the west still relevant? Jee ni sawa kuendelea kuwalaumu wakoloni (kama ambavyo Pan Africanists imekuwa tabia yao mara zote) kwa kutoendelea kwa Afrika kwa sasa, miaka 50+ baada ya UHURU? Jee ni vipi njia hii ina tija? Upande wa pili Mwalimu Nyerere alipendekeza falsafa ya kujitegemea…kwanini hata sasa bado Afrika yaonekana ni ngumu kujitegemea (hata basi kwa baadhi ya vitu tu)? kifanyike nini..? tunasongaje mbele toka hapa kati ya njia hizi mbili;- aidha kuendeleza lawama kwa mkoloni (Pan Africanism) au ya Mwalimu Nyerere kujitegemea kwa upande mwingine?

Profesa A Mwakikoti:  Karata ya lawama (‘blame game’ or rather, an excuse for development and growth that is cast toward the west) kwa makisio yangu si urasini-mantiki, ni irrational.  Tuna miaka 50 na zaidi ya Uhuru Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika.  Pan Africanist yoyote asiendelee kujificha kwa kivuli cha karata ya lawama kwa sasa..imetosha! Kabla ya uhuru na baada kwa miaka kadhaa sawa, ilionekana ina maana, mashiko, kuwalaumu magharibi.  Kwa sasa tujilaumu wenyewe kwa kutokuwa na mikakati kuchambua nini tunataka kufanikisha kama WaAfrika kwenye nchi zetu.  Mwalimu Nyerere aliona sawa kwamba, tuelekee kwenye wakati wa kujitegemea ambapo, kesho yetu haitaamuliwa tena na magharibi, kwa sisi kuzalisha wenyewe na kugawana kutokana na mipango yetu ya maendeleo ya Nchi.  Inanishangaza kwamba leo hii (mwaka 2019), bado sehemu kubwa ya bajeti yetu inategemea kupata michango (donations), mikopo na zaidi kutoka magharibi.
Wapi duniani ambapo mtu mzima wa fikra za urasini – mantiki (rational minded person) anapanga bajeti yake, akijumlishia kiasi anachotegemea kupata kama mchango toka kwa mjomba, jamaa na wapita njia watakaomsaidia kuzibia  pengo – balance ya bajeti yake..? hamna kitu kama hicho!
  Taasisi na hasa JICHO JIPYA lazima iweke kiwango – set standards, kuonyesha njia, kuishi kama watu wazima kwa kujitahidi kuwa na uhuru wa kiuchumi na kuiacha tabia hii ya karata ya lawama kwa magharibi.

10) Je, nini maoni yako juu ya Utamaduni – cultural revival? Unadhani kwa sasa lugha za kiasili (mfano Kihehe) zinaweza kuruhusiwa kama njia ya mawasilino pamoja na kiswahili na kiingereza hata kwenye matangazo ya Radio na TV, bila “woga” kuwa hiyo italeta / itachochea “ukabila”..?

Profesa A Mwakikoti:  Mimi ni mpenzi wa (proponent of) utalii wa kiutamaduni – local cultural tourism, na hivyo nafikiri lugha za kiasili nazo ziishi, ziendelee kuwepo ili kudumisha utamaduni asilia wa sehemu zetu.  Sio kitu cha ajabu kwamba katika kila lugha kuna maneno ambayo hayawezi kutafsirika kiufasaha kwa Kiswahili au Kiingereza (au kwa lugha nyingine yoyote) bila ya kupoteza maana yake asilia kwa sababu ya unadra wa utamaduni (culturally specific).  Kwa hiyo lugha asilia ziwe na nafasi katika mawasiliano kwa namna mbalimbali ikiwemo matangazo ili zidumishe utamaduni.  Ikiwa tunaweza kuwaheshimu watu waliohamasisha “utaifa” lakini wakati huo huo kuwa wazi (open) kwa mataifa mengine, kwanini isiwe hivyo kwa makabila pia, wakati huo huo ikiruhusu mahusiano chanya na makabila mengine?  Kwa kipimo changu, ukabila ni mbaya pale tu unapopelekea hali ya kabila kujiona lenyewe ni bora kuliko lingine/mengine, kwa kutumia vipimo vya kabila hilo kupima mambo yote ya makabila mengine.  Hii ni mfano mmoja wa fikra ambazo zinarithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, na kuchukuliwa kama ndiyo “kawaida”, sheria, bila ya kujiuliza maswali magumu kuhusu uhalali, ukweli, urasini – mantiki wake.

Jichojipya Think Anew: Na vipi hili linalosemekana kuwa kwa kufundisha kwa lugha ya Kiingereza, kumesababisha wanafunzi wengi katika ngazi ya sekondari, chuoni mpaka vyuo vikuu Tanzania kuwa na wakati mgumu kuelewa kiufasaha kinachofundishwa, ikisemekana kuwa ingekuwa ni kwa Kiswahili pengine mambo yangekuwa bora..?

Profesa  A Mwakikoti: Tatizo la lugha lipo. Kuna wanafunzi wa Tanzania wanao hangaika kujieleza kwa lugha ya Kiingereza. Ukweli ni kuwa, nchi nyingine mfano Mexico, Nchi za Waarabu na Asia, zinajifunza na kutumia lugha zao pamoja na Kiingereza wakati huo huo. Yahitajika balance, uwiano kwa lugha zote mbili. Hatuwezi tukatumia Kiswahili tu na kujitenga kwa mawasiliano ya kimataifa.
Wataalamu wanasema kwamba watoto wana uwezo wa kujifunza vizuri lugha mpaka 10 kwa wakati mmoja. Hivyo yaonyesha ni suala la msisitizo wetu sisi watu wazima, kupelekea lugha gani watoto wanajifunza. Ni suala la lugha tunazifundishaje.

Jichojipya -Think Anew: Ndiyo…katika moja ya hotuba zake ya miaka ya 1990, Baba wa Taifa Mwl Nyerere  akizungumzia suala hilo alisema, sisi Tanzania tumebarikiwa kuwa na “Viswahili” vyote viwili, cha kwetu na cha dunia – akimaanisha Kiingereza, akaongeza kuwa tujifunze vyote na tutumie vyote. Kwamba juhudi za kuendeleza Kiswahili chetu, sisimaanishe kudhoofisha Kiingereza, la hasha.
Hivyo ni kweli, ni suala zaidi la njia, jinsi ya ufundishaji.

11) Hapa Tanzania, kuna watu wachache sana ambao wanajulikana wazi katika jamii kuwa ni WanafikraHuru – wanaoishi bila dini (na ndiyo sababu ya kuwatafuta hao na kuweka kumbukumbu za maisha yao – kama alivyofanya Mwana falsafa Henry Odera Oruka miaka ya zamani ya 70)…
Jee kuna WanafikraHuru wengine kama wewe ambao unawajua? (Hata mzee Kingunge tulimuuliza swahi hili) na jee una mawasiliano, link na WanafikraHuru wengine wowote duniani? (Mzee Kingunge alituambia yeye alikuwa peke yake hata katikati ya Ma “comrade” wenzake – yeye akiwa Marxian anayekubaliana tu na dhana ya nguvu za ukinzani  – “dialectic approach” katika kuichambua jamii, lakini kamwe hakuwa Mmarxist kama ambavyo makomredi wenziwe walivyomdhania kuwa..!)

Profesa A Mwakikoti:  Ninawafahamu wachache WanafikraHuru, hasa wa Marekani ambao nina link na kukutana nao mara chache kadhaa.  Wachache hao ni wanachama wa “Freedom From Religion Foundation” (FFrF), na “American Humanist Association” ambapo nami ni mwanachama.  Ninatumiwa matoleo/maandishi ya Taasisi hizo, na nimewahi kuudhuria mikutano waliyoiandaa.  Ninafikiri ni muhimu sana kufanya utafiti mfano kwa hapa Tanzania, kujua idadi ya WanafikraHuru hapa, ingawa katika sensa, Mwalimu Nyerere alisema hakukuwa na haja ya kuwauliza watu imani/dini zao, akisema hiyo ni kazi ya viongozi wa dini kujua waumini wao.  Lakini, hili ni jibu sahihi?  Kutakuwa na madhala gani kuwa na taarifa hizo kwa Taifa kama swali hilo lingeulizwa? Hata hivyo kwa sasa, JICHO JIPYA yaweza kutafuta njia ya kiutafiti kukusanya taarifa muhimu ambazo zitatumika kwa malengo yenye tija kwa jamii.

12 ) Kama MwanafikraHuru, unatoa ushauri gani katika kukuza Sayansi na Tekinolojia, kutoka ngazi ya chini na sekta isiyo rasmi?

Profesa A Mwakikoti:  Sayansi na Tekinolojia na mambo mengineyo ya kielimu yenye tija kwa jamii, lazima yaangaliwe kwa ufasaha. Utafiti ufanyike, halafu mkakati na kupima wapi itapofaa ktk mpango wa muda mrefu.  Elimu iwe ni kwa faida ya jamii, isiwe elimu kwa maana ya elimu tu basi.  Nina maanisha elimu yoyote ya maana lazima iwe na mpango wa vipi itainufaisha jamii – Mwanafunzi na jamii kwa ujumla.  Bila ya utafiti wa kiufasaha na mipango, jamii yaweza kuishia kuzalisha wahitimu wa mashahada katika nyanza zilezile, huku ikishindwa kuwaajiri au kuwawezesha (empower) wajiajiri wenyewe (kama wajasiliamali).  Elimu ya aina yoyote lazima iwe inakwenda na uhalisia / hali halisi – pragmatic, na wanafunzi wajue mwanzo kabisa kabla wataitumia vipi elimu hiyo kivitendo, mapema wanapoanza safari ya kusoma hicho wanachosomea.  Zaidi ni kuwa, elimu isiyotumika baada ya kuhitimu ni upotevu wa rasilimali, mbaya zaidi kuliko hata ya kutoipata.   Elimu ya Sayansi na Tekinologia ndio mchezo wa sasa, hatuwezi kuishi bila, na ni lazima ikuzwe.  Na uko sawa kabisa, ukuzaji huo lazima uwe kwa ngazi zote; kwa sekta rasmi na ile isiyo rasmi.  Sekta rasmi ishughulikie zaidi utafiti ulio kiuhalisia, pragmatic, kwa lengo la kufikia kwa uvumbuzi utokanao na utafiti.  Lakini pia ni muhimu kusema kwamba tuna Watanzania vijana walio na vipaji vya kuzaliwa hata kama wana elimu ya chini, au hawakwenda shule kabisa.  Cha ajabu ni kwamba vijana hawa wamevumbua na kutengenea kila aina ya vitu ambavyo wengi wetu hatuna habari.  Mfano mzuri ni mmojawapo wa JICHO JIPYA, Bwana Ntubanga Beleng’anyi –ambaye ametengeneza kutoka mwanzo garimoto linalofanya kazi.  Watu kama hawa, yafaa wawezeshwe – wapewe incentive and encouragement it waendelee na uvumbuzi wao.

13) Kwa maoni yako kama MwanafikraHuru, unadhani kuna haja ya kuwa na vijiji vinavyo lea na kukuza sayansi na tekinolojia, kama ilivyokuwa kwa kijiji cha Isansa kule mbozi kwa suala la kilimo na ufugaji wa kiushirika? Jee kuwe na “Silicon-valley ya Tanzania? Kama Ilivyowahi kufikiriwa siku za nyuma na Prof Shayo..?

Profesa A Mwakikoti:  Binafsi sielewi sana kuhusu Isansa – Mbozi ulivyokuwa, ila kwa wazo la kulea na kukuza sayansi na tekinolojia hili ni muhimu.  Lakini kabla ya hapo, mtu lazima ajiulize kwanza kwanini tunahitaji sayansi na tekinolojia—ili iweje – kwa kutaka matokeo gani – for what end results? Jee tumefanya tafiti zozote kwa hilo kwamba, ikiwa tutawaelimisha / kuwapa mafunzo vijana  elfu moja, asilimia fulani itakwenda kuajiriwa kwenye viwanda fulani kadhaa ambavyo tuna uhakika huo, na asilimia nyingine itaanzisha shughuli zao wenyewe katika maeneo ya sayansi na tekinolojia? Kama hatujafanya hivyo, hatujakusanya taarifa hizo, kwanini basi twende kichwa – kichwa kwenye elimu hiyo/mafunzo hayo?  Kwa sasa tunaishi katika zana za ulimwengu wa tekinolojia ambapo, inawezekana kabisa kutafuta majibu, matokeo kwa kitu chochote kabla ya kupeleka nguvu na pesa zetu kwenye kitu hicho.

Jichojipya Think Anew: Isansa ilikuwa ni kijiji ambacho Mwl Nyerere alikiona ni mfano wa alichotaka kiwe kwa siasa ya ujamaa, ushirika na kujitegemea. Kilikuwa huko Mbozi mkoani Mbeya.

14) Mwl, Profesa, vitabu vyasemekana kuwa ni virutubisho vya ubongo. Wewe kama Mwana fikraHuru, una mapendekezo gani kuhusu nini kifanyike kuchochea na kuendeleza tabia ya kujisomea vitabu ili iwe “utamaduni” hapa Tanzania, nje ya kusoma ili tu kufaulu mitihani shuleni?
Na kwako binafsi, ni kitabu gani ambacho unadhani baada ya kukisoma kilichochea wewe kuwa Mwana fikraHuru kama ulivyo sasa?

Profesa A Mwakikoti: Kwa kweli tabia ya kupenda kujisomea vitabu inajengeka kwa mafunzo ya malezi, haiji tu yenyewe.  Kwa dunia ya leo kuna namna mbalimbali ambazo mtu anaweza kusoma vitabu, vingi, na kwa urahisi.  Tabia ya kujisomea vitabu kwa vijana katika jamii nyingi inaonekana kupotea. Lakini ni kwa kusoma vitabu ndio tunapata kujua mambo mengi zaidi na zaidi yaliyo katika jamii.  Ikiwa kusoma kitabu yaonekana inachosha – boredom, mtu anaweza badala yake kusikiliza vitabu kwa njia ya sauti – kama audio books – wakati huohuo akifanya mengineyo mfano kutembea au kuendesha gali.  Kwangu binafsi, Biblia ni kitabu kimojawapo kilichonitoa / fukuza nje ya Ukristo, Kiukweli kabisa.  Makinzano – contradictions zilizomo mule zatosha kabisa kumsukuma mtu nje ya imani.  Halafu vitabu kama The God Delusion cha Richard Dawkins, God is not Great: How Religion Poisons Everything cha Christopher Hitchens, na Misquoting Jesus: The Story Behind Who Changed the Bible and Why cha Bart D. Ehrman, vilikuwa vitabu vyangu vya kwanza kuvisoma na kupata ahueni kutoka miaka yangu ya mahangaiko katika ukristo.  Baada ya hapo zaidi, nimesoma vitabu kadhaa kutoka kwa waandishi mahili. Kusoma vitabu yaleta haueni / afueni – comforting –  inajenga na kusaidia kuweka sawa uelewa, kwa maswali ambayo Mwana fikraHuru daima anajiuliza na kuwa na kiu isiyokatika ya kutaka majibu.

Jichojipya – Think Anew: Mwl, kitabu hiki ambacho Mzee Kingunge alitueleza tulipomhoji kuwa alipokisoma ndipo akang’amua kuwa alaa, kumbe ni binadamu ndiyo wametengeneza miungu kwa mawazo yao..! ni kitabu cha Ludwig Feuerbach “Essence of Christianity”, nyuma kinasoma hivi: “did god create man? Or did man create god”? – nani alimuumba nani? Mungu kaumba binadamu, au binadamu kamuumba mungu?

15) Profesa, Nini maoni yako juu ya nadharia ya Mtafiti charles Darwin, ya zamadamu…kama ilivyo kwenye kitabu chake “origin of species”?

Profesa A Mwakikoti:
Binafsi ninafikiri nadharia ya zamadamu – evolution and the origin of species ya Charles Darwin ina mashiko kwa maelezo ya kifikra – urasini mantiki kuliko imani za kufikirika bila sayansi, mfano imani ya kuwepo kwa Mungu. Ijulikane kuwa, mimi kama mwana sociolojia na mwanafikra huru, nina amini uwepo kwa miungu iliyotengenezwa na binadamu katika jamii nyingi, kwa taswira (image) ya jamii yenyewe.

16)  Profesa, Wewe kama MwanafikraHuru, unafikiri ni muhimu kuzisoma dini mbalimbali kwa ulinganisho (comparative religion study) pamoja ya kuwa wewe si muumini wa mojawapo yoyote?

Profesa A Mwakikoti:  Kuzisoma dini mbalimbali, kwangu mimi naona inafaa kama wewe ni mchambuzi au mtu wa midahalo kwa mada hizo.  Elimu hiyo inasaidia kuwaelewa watu na imani zao vizuri zaidi, na hii inapelekea kujua mitazamo yao. Nilipokuwa Pastor, niliwahamasisha waumini kusoma na kuzijua dini zingine—ila kusudio langu lilikuwa kujua jinsi ya kubishana na kushinda midahalo ninapofanya hivyo, na wazungumzaji wa dini au mahehebu mengine. Sijutii safari yangu iliyonipeleka kusomea elimu ya dini – Thiolojia. Leo nikiangalia nyuma, ninajua ilichangia kunisaidia niweze kuidadisi imani ya ukristo kwa undani zaidi.  Pia, kusoma dini mbalimbali kunamfanya mtu awajue vizuri wafuasi wa dini hizo, na hiyo inasaidia katika kuwasiliana nao.

Ndoto ya watoto kutengeneza galimotokali wakiwa wakubwa, ilitimia kwa Ntubanga Beleng'anyi Scott Douglas Jacobsen In-Sight Publishing

Ndoto ya watoto kutengeneza galimotokali wakiwa wakubwa, ilitimia kwa Ntubanga Beleng’anyi.

17) Mwl Profesa, kama MwanafikraHuru, una maoni gani kuhusu “Hero – worship”? Kumuona shujaa hana kosa…Yupo sawa kwa kila kitu…lini tutaanza kuwa “Wanafunzi” wa Mwalimu (na wazuri kwa hilo!) badala ya kuendelea kuwa “Wafuasi” ritual disciples – Kwa maana ya kuwa ni vipi tunaweza kumuangalia Mwalimu kifalsafa zaidi, critically, badala ya sasa ambavyo anaonekana ni political saint,“Mtawa”?

Prof A Mwakikoti:  WanafikraHuru mara zote lazima waangalie kitu chochote kwa jicho la kinyonga (la kuzunguka pande zote) – critical mind.  Tunapomuheshimu mtu mpaka hali ya kumuabudu – worship tunakuwa hatuna tofauti na wale waliotengeneza miungu katika jamii zao.  Viongozi wakubwa – Great leaders wapewe heshima zao na wawe kioo / kiwango / kipimo wakati tuna chambua na kuona ni nini wametusaidia kujifunza, na vivohivyo iwe kwa Mwalimu Julius K. Nyerere.  Pamoja na heshima kubwa niliyonayo kwa Mwalimu Nyerere, lakini alifanya makosa pia na yeye mwenyewe alikubali hilo.  Wakati anastahili sifa kwa mchango wake mkubwa kwa Taifa Tanzania, ni budi tujifunze na kuchambua vitu vile ambavyo tunaweza kumuiga, na kuachana na vile ambavyo tunajua haviwezi tena kuwa applicable -kufanyika kwa jamii yetu ya leo, au tuseme vibaki tu kwenye maktaba za kumbukumbu – Museums.

Jichojipya – Think Anew: Ndio, Mwalimu Nyerere mwenyewe kwa mafundisho yake mbalimbali kupitia hotuba na maandishi alionyesha kuwa  jamii ni dynamic..lazima ibadilike kuendana na changamoto mpya. Alilishauri hata kanisa katoliki kuwa tayari kwa mabadiliko kwa sababu kwa maneno yake mwenyewe, “dunia inahitaji mawazo mapya”, na “maendeleo ni uasi”! – Hotuba yake mwaka 1970 katika mkutano wa masista wa kanisa, Maryknoll  New York Marekani). Yeye mwenyewe alianzisha mabadiliko kadhaa makubwa ya kijamii wakati wake, hakuna haja ya kumfanya“dogma.” alikwenda (na alitaka) mabadiliko ya wakati.

18) (a) Profesa, Kutokana na maisha yako kama Mwana fikraHuru, unapopata matatizo kimaisha, watu wenye dini uenda kupata faraja – consolation aidha kanisani, msikitini au kwa waganga wa kienyeji au hata wapiga ramli, sasa kwako wewe MwanafikraHuru unakwenda wapi kwa hilo? Jee si ni mzigo mzito sana kwako? Umewezaje kuendana (to cope) na hali hiyo ya kuwa peke yako muda wote na bado umebaki na akili timamu?
(b) Na kama MwanafikraHuru, unadhani ni wazo zuri kwa MwanafikraHuru kuacha maandishi – Will ili kwamba azikwe nje ya utaratibu wa dini kama vilevile alivyoishi maisha yake nje ya mila / desturi hizo?

Profesa A Mwakikoti:  Bahati nzuri hata nilipokuwa kwenye dini – ya Ukristo, sikuwa nakwenda kwa mtu au taasisi kupata faraja, ingawa niliuliza wengine kama wangehitaji msaada wangu katika kukabiliana na hali kama hizo. Yangu nilibaki nayo mwenyewe na kuwaeleza marafiki wachache ilipotokea hivyo – wengi wa hao hao marafiki wachache walinigeuka wakaniacha pale nilipoachana na dini na kuwa mwanafikra huru. Nimewahi kuulizwa swali hili linalokwendana na hilo, kwamba ninafanya maandalizi gani kabla sijakutana na kifo, hasa sasa ambapo mimi si muumini – I am an unbeliever? Jibu langu ni kuwa, wala hili halinihangaishi akili, kwa kuwa nina amini maisha ni haya haya, ndiyo pekee tuliyonayo, hamna mengine baada ya haya.

Na ninafikiri MwanfikraHuru ni budi aandike andiko la Will  ili kupunguza utata wa kifamilia, kujua watafanyaje na wewe, mwili wako, pale utakapokufa.  Ni vizuri kuandika, hata kama maandishi yako hayatapewa uzito – kutochukuliwa serious, na wale watakaobaki, hasa pale inapokuwa wao ni waumini wa dini.  Ikitokea hawatataka kufuata mapendekezo ya will yangu, basi, wacha wafanye inavyowapendeza wao, haitabadili mimi ni nani, yote kwa yote nitakuwa tayari mfu, haitabadili kitu.

An Interview to a Tanzanian Emeritus Professor Alex L. Mwakikoti on Living Without a Religion and More 3 Scott Douglas Jacobsen In-Sight Publishing

Jichojipya-Think Anew: Kuna haja kwa WanafikraHuku kuanza kukutana mara kwa mara, kufahamiana. Hii itaondoa “upweke” ambao kila mmoja kati yetu anaupata, akiwa peke yake, kivyake. Tupo wachache lakini ndo tupo. Mzee Kingunge alishauri hivyo. Tutumaini kujenga jamii ya WanafikraHuru tukisaidiana kama ambavyo ni Ubinadamu ambao ni wanyama wanaohitaji kuishi pamoja – human animal social being. Zaidi ya hilo kuna wazo la kuanzisha Humanist Celebrants, itakuwa ni mbadala kwa WanafikraHuru na wengine pia, ambao wangetaka kufanya ndoa za Bomani zikienda na sherehe/kumbukumbu zisizo za kidini. Vilevile kwa coming out celebration (mbadala wa ubatizo) kwa watoto. Na pia ikiwa mtu ameacha Will kwa maandishi kwa maziko yake bila kuwepo na mila/desturi za kidini. Inawezekana kabisa kuzaliwa, kukua, kuishi, kuingia kwenye ndoa, kuwa Mzee, kufa na hata kuzikwa bila ya mila na desturi za kidini kukushurutisha. WanafikraHuru yabidi kuya-anzisha haya kati yetu katika jamii hii. Wakati ni huu. Tusaidiane kuweka msingi kwa freethinkers wa vizazi vijavyo, miaka 50 mpaka 100 baada yetu. Mzee Kingunge kwenye mahojiano yake nasi, alitushauri tuwe tunakutana mara kwa mara. Huo ndio “wosia” wake kwetu.

19) Mwisho kwa leo, umeishi maisha marefu kama MwanaFikraHuru, kuna siri gani juu ya kuishi vizuri, muda mrefu, maisha yenye mchango mzuri kwako binafsi na kwa  jamii – productive and useful life?
(b) Neno lolote la mwisho la kuwahamasisha chipukizi, “Young Africans” ambao ni Freethinkers kujifunza toka kwako wewe “Simba – Lion” shujaa wa maisha haya ya kuishi vizuri kwa maadili bila dini…“Living without religion”..?

Profesa A Mwakikoti:  Kwanza, kwa miaka takriban 10 tu ya kuwa MwanafikraHuru si muda mrefu. Lakini kwa kipindi hicho cha kuwa MwanafikraHuru, Ninashukuru kwa kweli kuwa hivyo. Nimepata Uhuru kwa kuwa MwanafikraHuru, Uhuru kutoka kutawaliwa kama “mtumwa” wa dini kwa miaka karibu 50. Siri? Sidhani kama kuna siri yoyote, ila najua kuwa kuishi maisha yako bila woga wowote ni mojawapo ya fanikio la kuwa MwanafikraHuru.  Kwepa hisia ya kutaka kuwabadili wengine wawe kama wewe, badala yake ishi tu maisha yako bila imani ya dini yoyote, na wengine watakutafuta na kutaka kujua zaidi, nini una amini.  Na kama nilivyokwisha sema, vijana ndio chachu – champion wa mabadiliko kwenye jamii, watafute njia zao wenyewe kuongoza fikra za urasini-mantiki critical & rational thinking ambayo ndiyo njia MwanafikraHuru uitumia katika kuyakabili matukio ya maisha.

                                 Shukrani sana Mwl Profesa A Mwakikoti

An Interview to a Tanzanian Emeritus Professor Alex L. Mwakikoti on Living Without a Religion and More 4 Scott Douglas Jacobsen In-Sight Publishing

Ndoto ya utoto ya Ntubanga Beleng’anyi kutengeneza gali ukubwani iliyotimia.

Jichojipya-Think Anew: Tunajiona wenye bahati tena, kwa kuweza kuwa na haya mahojiano nadra sana ya kifalsafa na Mwl Profesa, mahojiano ya kiwango  kile-kile, upeo ule-ule tuliofanya na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru. Shukrani sana Mwalimu.

Wapendwa, tunawashukuru wote kwa interest na attention yenu. Tafadhalini, fuatilieni Jichojipya katika social media sites, tukiendelea kuwatambua, kuwaibua na kuwaunganisha WanafikraHuru wa Kitanzania – “identify, unearth and connect Tanzanian freethinkers”. Hawa ni watu nadra wadadisi wasiochoka kujiuliza maswali, ambao kwa kutumia njia ya kusoma na kujisomea vitabu, wakang’amua kuwa kumbe inawezekana kabisa kuishi maisha ya Maadili bila dini, ukiongozwa na urasini -mantiki usio na woga wa kuhoji chochote na usioamini imani za kusadikika, “supernatural” hata zile ambazo ni za kidini. Asanteni tutakutana kwenye mahojiano mengine..! Wanafikra huru wapo, hata hapa Tanzania, ni haki yako kujiuliza maswali bila kuchoka, haupo peke yako, na wengine kama wewe wapo, kujiuliza maswali siyo “kuchanganyikiwa”, ni kielelezo cha juu kabisa – fullest expression cha Ubinadamu wako..!
Ni Nsajigwa I (Nsa’Sam) Mwasokwa and Isakwisa A Lucas, jichojipya-Think Anew..!
+255767437643    +255714437643   + 255742674383 +255754326296 jichojipya@gmail.com

Vitabu vilivyoambatana na mahojiano haya: –
1) Eupraxsophy – Living without religion – Mwandishi Profesa Paul Kurtz,
2) The Tanzania (1977) constitution, toleo la 2005
3) Essence of Christianity – Mwandishi Ludwig Feuerbach.

Appendix I: Footnotes

[1] Individual Publication Date: March 22, 2019: http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

Appendix II: Citation Style Listing

American Medical Association (AMA): Mwasokwa I, Isakwisa A Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia? [Online].March 2019; 1(A). Available from: http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

American Psychological Association (APA, 6th Edition, 2010): Mwasokwa, N. I., Isakwisa, L. A. (2019, March 22). Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?Retrieved from http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

Brazilian National Standards (ABNT): MWASOKWA, N.I.; ISAKWISA, L.A., Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia? African Freethinker. 1.A, March. 2019. <http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili>.

Chicago/Turabian, Author-Date (16th Edition): Mwasokwa, N.I., Lucas A. Isakwisa, Isakwisa. 2019. “Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?.African Freethinker. 1.A. http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

Chicago/Turabian, Humanities (16th Edition): Mwasokwa, N.I., Lucas A. Isakwisa “Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?.African Freethinker. 1.A (March 2019). http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

Harvard: Mwasokwa, N. I. and Isakwisa, L. A. 2019, ‘Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?, African Freethinker, vol. 1.A. Available from: <http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili>.

Harvard, Australian: Mwasokwa, NI & Isakwisa, LA 2019, ‘Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?, African Freethinker, vol. 1.A., http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

Modern Language Association (MLA, 7th Edition, 2009): Mwasokwa, N. I. and Isakwisa, L. A. “Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia?.” African Freethinker 1.A (2019):March. 2019. Web. <http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili>.

Vancouver/ICMJE: Mwasokwa NI and Isakwisa LA Mahojiano Na Profesa Alex L Mwakikoti Juu Ya Maisha Ya “Maadili Bila Dini” Anayoishi, Na Mengineyo – Jee Inawezekana Kwa Wengine Pia? [Internet]. (2019, March; 1(A). Available from: http://www.in-sightjournal.com/Mwakikoti-kiswahili.

License and Copyright

License

In-Sight Publishing and African Freethinker by Scott Douglas Jacobsen is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.
Based on a work at www.in-sightjournal.com.

Copyright

© Scott Douglas Jacobsen, and In-Sight Publishing and African Freethinker 2012-2019. Unauthorized use and/or duplication of this material without express and written permission from this site’s author and/or owner is strictly prohibited. Excerpts and links may be used, provided that full and clear credit is given to Scott Douglas Jacobsen, and In-Sight Publishing and African Freethinker with appropriate and specific direction to the original content.  All interviewees co-copyright their material and may disseminate for their independent purposes.

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: